Nafahamu nina watu wangu wa nguvu ambao wao furaha yao siku zote ni kuendesha magari mazuri, na mara nyingi hawapendi kukaa nayo muda mrefu, hupendelea kubadilisha mara kwa mara. Mtandao wa www.autotrader.com umetoa list ya gari 5 za Luxury zinazotarajiwa kutoka 2016.
1- Acura NSX hii ni moja kati ya gari za kifahari zitakazotoka 2016 na gharama yake inatajwa kufikia dola 150000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 330.
2- Audi TT ni moja kati ya kampuni ambazo zinatajwa kuwa zinatengeneza magari mazuri, ila ili kuweza kuendesha Audi TT2016 utahitaji kulipa kiasi cha dola 47,400 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 100.
3- Buick Cascada hii ni moja ya magari ya Luxury ambayo yametajwa kuwa yataingia sokoni 2016, ukihitaji kulimiliki ni lazima huwe na dola 35000 mkononi ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 70 .
4- Cadillac CT6 ni moja kati ya magari yanayotajwa kuingia sokoni 2016 , bei rasmi haijatajwa ila kama utakuwa na dola 82,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 170 basi itakuwa ni rahisi kwako kulimiliki.
5- Infiniti Q60 gharama yake inatajwa kuja kufikia dola 42,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 90.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni