.

Ijumaa, 24 Juni 2016

Max amefunguka ishu ya Young dee kuonekana kumdiss Babu tale kwenye posti ya Chid benz


Juzi ilikuwa ni siku ya furaha kwa mashabiki wa mziki wa Bongo fleva baada ya kumwona msanii wao Young dee kurudiana na Management yake ya MDB ambayo iko chini ya Max na kukiri kwamba hatokuja kutumia tena madawa ya kulevya.

Baada ya kuongea na wandishi wa Habari Escape One jijini Dar es Salaam, rapper huyo aliwaomba radhi watanzania kwa vitendo hivyo na kuahidi kubadilika.

Alidai kuwa ni marafiki ndio waliompoteza na kumuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Tukirudi nyuma kidogo Young dee alishatrend kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumdiss Babu tale kwa namna alivyo mpost Chid Benz, Management yake imefunguka kuhusu isue hiyo nakusema Young dee alkuwa kwenye giza.

Akiongea na 255 Max amesema kwamba mtazamo wa Young dee ulikuwa kwenye giza na alipoona mtu yeyote anataka kuleta nuru hujisikia vibaya, vilevile aliongelea hali pia aliyokuwa nayo d wakati anaposti ilikuwa ni ya madawa ya kulevya

“Unapokuwa kwenye mazingira machafu alafu ukasikia mtu anauongelea uchafu unatamani mtu yeyote asiuongelee uchafu…..mtazamo wa young dee ni kwamba mimi nilikuwa kwenye giza na ninapoona mtu yeyote anataka kuleta nuru najisikia vibaya binafsi, halichokiongea hakikuwa kitu binafsi kwamba anampointi babu tale vidole…………………………………

Babu tale ni mtu mmoja ambaye amesaidia hizi harakati na mpaka kesho Babu tale ni mtu mmoja ambaye yuko poa sana na d, hata juzi aliniambia kama kuna kitu chochote ambacho mnahitaji mimi niwe msaada kwa d niko radhi” Alisema Maximilian

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni