Kama wewe ni mmoja kati ya watumiaji wa mitandao kwa kutumia smartphone yako, basi mtandao wa YouTube umetangaza maboresho katika application yao kwa watumiaji wa simu za mkononi.
YouTube wametangaza kuboresha application yao ya YouTube inayotumika katika smartphone, sasa unaweza kuweka video za YouTube live streaming kupitia simu ya mkononi, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza button katika simu yako na video unayorekodi moja kwa moja itaenda YouTube.
Maboresho hayo ya YouTube kwa application za simu za mkononi, unaweza ukaifananisha na ile application ya mtandao wa Periscopena itakuwa na option ya viewers kuweka comment zao kama kawaida. Mfumo huo wa live streaming kwa simu za mkononi waYouTube unaitwa ‘YouTube Connect’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni