.

Jumatatu, 20 Juni 2016

Nuh Mziwanda asema hatomuomba msamaha Shilole, Atoboa sababu yakumuita ‘Mcheza show’


Mziwanda kafunguka leo kupitia Planet Bongo kuwa anajua Ex wake shilole alidhani atashuka baada ya kuachana kwao ili arudi kumuomba msamaha lakini hilo halitatokea kamwe.

Juzi kati shilole alipost Instagram kuwa aache kutumia mgongo wake kutoka kama vipi arudi aombe msamaha.

Wiki iliyopita Nuh mziwanda alinukuliwa akisema hawezi kushindana na Ex wake Shilole kwa kile alichosema yeye ni mwanamuziki shishi ni mcheza show.

Akifafanua kauli hiyo kwenye Planet Bongo amesema aliongea hivyo ili kumfahamisha Ex wake huyo kuwa hawawezi kulingana hata siku moja kwasababu yeye ni msanii kamili anayeweza kupiga piano, kutengeneza beat (Producer), kuimba na kufanya mambo mengi kwenye music tofauti na yeye (Shilole).
Anasema shilole amekuwa akifanya fitna za kila aina ikiwemo kupitia marafiki zake ili ashuke na amefanikiwa kwa kiasi chake lakini anapenda kumfahamisha kuwa haya ni maisha kuna kupanda na kushuka.

Shilole alipotafutwa kuhusu issue hiyo alisema neno moja tu “NO Comment”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni