.

Jumatatu, 20 Juni 2016

Diamond platnumz azidi kuwapa raha mashabiki wake, ameandika haya kwenye ukurasa wa Instagram


Msanii wa Bongo fleva Diamond platnumz anazidi kuwapa presha mashabiki wake kuhusu ujio wa video ya wimbo wake aliofanya na P square kutoka nchini Nigeria.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Diamond platnumz amepost picha akiwa na kundi la P Square pamoja na uongozi wake, huku wakiangalia kazi hiyo kama kufanya mapitio na kuandika kuwa anasikia harufu ya hit song.

Damn! am Smelling a Hit!!! subscribe on my Youtube Channel now named DIAMONDPLATNUMZ so that you can be the first Witness! Cc @peterpsquare@rudeboypsquare #SiMbaKaseMa aliandika Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram

Haijajulikana video hiyo itaachiwa mda gani ila ameshaanza kuwaweka sawa mashabiki wake kukaa tayari na kuwa karibu na mitandao yake kwa ajili ya kazi hiyo aliyofanya na wasanii hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni