.

Ijumaa, 24 Juni 2016

Chris Brown afunguliwa mashitaka kwa kumpiga meneja wake


Chris brown anazidi kuwashangaza mashabiki wake kwa kutawalia na matatizo mengi ambayo yanamfanya kufunguliwa mashitaka mbalimbali, hivi karibuni ameshitakiwa na jamaa aliyemwajiri kwa ajili ya kurekebisha mtazamo wa mashabiki kwa Chris brown baada ya kumpiga Rihhana, leo anamshataki Chris kwa kumpa kipigo kama alichompa Rihhana.

Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Chris brown amemshushia kipigo Meneja wake aliye mwajiri mwaka 2012 ambaye ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya kubadilisha mtazamo wa mashabiki kwa Chrisbrown, kulipa madeni ambayo brown alikuwa anadaiwa pamoja na kumwondoa kwenye maswala ya madawa ya kulevya.

Mike G ameeleza kuwa bila sababu yoyote ile ya uchochezi, Chris alimchukua mpaka chumbani na kikatili akaanza kumshambulia kwa ngumi nyingi za usoni na shingoni ambavyo vilimfanya kujikuta akiwa emegerncy room.

Katika mashitaka aliyoyafungua meneja wake amesema kwamba badala ya Chris brown kuonesha majuto na kuomba samahani kwa aliyofanya, Chris ndio kwanza anaonyesha majivuno kwenye mitandao ya kijamii na kwa marafiki zake kwa kumpiga na kutamba kwa kuwaambia watu ambao anafanya nao kazi kwenye tour yake kwamba nao wakitoka nje ya mstari atawashushia kipigo kama alichopata Mike G.

Hata hivyo Mike G amesema kuwa hasira hizo zilizomfanya Brown kumpiga zimetokana na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni