.

Jumamosi, 10 Juni 2017

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2017 HAYA HAPA


Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene ametoa idadi hiyo leo Juni 9, mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Amesema kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 pekee waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Amesema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu kwa vigezo vyote vya msingi ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa Julai 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," amesema Simbachawene.

===========

Kuangalia Majina Bofya Hapo chini

2.Watakaochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Pili 2017

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni