Vanessa Mdee na Jux ni wakali wa Bongo Fleva ambao inafahamika fika kuwa wapo katika mahusiano ya kimapenzi, na kama ijulikanavyo kwa watu maarufu, ni mengi ambayo yanazungumzwa kuhusu wao, ikiwa ni yenye ukweli na hata yasio na ukweli.
Kwahiyo kama wapenzi ni lazima kuwe na mambo ambayo kila mmoja anaweza kuyasikia kuhusu mwenza wake na asipendezwe nayo na vitu kama hivyo.
Kupitia Perfect255, Jux ameamua kushare na sisi kitu ambacho alikisikia kuhusu mpenzi wake Vanessa Mdee na kikatokea kumuumiza sana kuliko mambo yote ambayo amewahi kuyasikia kuhusu mpenzi wake huyo.
Jux ametusanua kuwa kitendo cha jina la mpenzi wake huyo kutajwa kwenye list ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya kilimuumiza sana, kwasababu ni mtu ambaye anamjua vizuri na wala hajawahi hata kuhisi kuwa Vee anajihusisha na madawa.
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni