Akon, Wizkid, Don Jazzy, Davido na Oliver Mtukuzi watamba kwenye orodha ya wasanii Afrika wanaongoza kwa mtonyo.
Kikubwa ambacho jarida hilo la Forbes Africa wameangalia mpaka kupata listi hiyo ya wasanii kumi wanaongoza kwa mitonyo ni kwa kuangalia vigezo kama thamani ya endorsement zao wanazozipata, umaarufu, viwango vya show zao wanazofanya, mauzo, tuzo, watazamaji wako kwenye chaneli za Youtube, kutokea kwenye magazeti, kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wengine, uwekezaji na uwepo wao katika mitandao ya kijamii.
1.AKON
Akon anaingia kwenye listi hii kutokana na mauzo ya album zake takribani milioni 35 zilizouzwa kila pande ya dunia, kingine kikubwa ni kwamba Akon ameshajinyakulia grammy tano huku akiwa ameingiza ngoma 45 katika chati za ya Billboard hot 100
2. BLACK COFFEE, AFRIKA KUSINI
Maarufu sana kutokana na tuzo ambazo amewahi kujishindia kama BET, wengi wanamfahamu kwa jina kamili la Nkosinathi Maphumulo , kubwa zaidi Black coffee ameingia kwenye album mpya ya Drake “More Life” ambayo inafanya vizuri sokoni.
3. HUGH MASEKELA, AFRIKA KUSINI
Alizaliwa witbank, mashariki mwa Johannesburg, Hugh Masekela alshafanya takribani album 43 ambazo zote hizo aliwahi kuperforme na wasanii wakubwa kama Marvin gaye, Stive Wonder, Miriam Makeba na wengine kibao.
4. DON JAZZY, NIGERIA
Producer kutoka nchini Nigeria ambaye amejibebea mafanikio makubwa katika game ya muziki afrika mpaka Marekani ambapo alifanikiwa kuja na label yake ya Mavins ambayo nayo imebeba vichwa vingi vikubwa vinavyofanya vizuri Afrka, Do Jazzy alianza tasnia ya muziki tangu yuko mdogo kanisani mpaka kufikia hatua hii aliyokuwa nayo sasa.
5. TINASHE, ZIMBABWEAN-AMERICAN
Maarufu na ngoma kama ya “2 On aliyomshirikisha School Boy” pamoja na “How long” ya davido, Tinashe ni mchanganyiko Mzimbwabwe pamoja na America, vilevile ni mwandishi mzuri wa nyimbo, muimbaji, muigizaji pamoja na dancer. alishashinda tuzo kibao kupitia wimbo wake wa “2 On”. Tinashe aliingia kwenye listi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutokea katika jarida la Play Boy bila kukaa utupu.
6. JIDENNA, NIGERIAN-AMERICAN
Mzee wa Classic, anajulikana kama Jidenna Theodore Mobisson, mbali na kuwa maarufu katika tasnia ya muziki, Jiddena angekuwa ni moja ya masound Engineer, amejizolea umaarufu na ngoma yake ya Classic Man, Yoga, Long Live Chief na zingine kibao.
7. WIZKID, NIGERIA
Moja ya wasanii afrika wanaofanya vizuri Duniani na kugusa kila mioyo ya wapenda muziki, ameingia kwenye tuzo nyingi kubwa duniani kupitia wimbo wa “One Dance” alioshirikishwa na Drake pamoja na “Come Closer” anayotamba nayo kwa sasa.
8. DAVIDO, NIGERIA
Moja ya washikaji ambao wamepigana sana kufikia hatua ambayo yupo nayo sasa akiwa na ngoma nyingi kali na kutengeneza njia kibao kwa muziki wa Afrika kuchomoza zaidi. alishapiga kolabo na msanii kutoka Bongo, Diamond platnumz.
9. SARKODIE, GHANA
Alianza kama Underground rapper katika tasnia ya muziki wa kiafrika mpaka kufikia hatua ya mghana wa kwanza kushinda tuzo ya BET, maarufu na ngoma “No kissing Baby”, “Pain Killer”.
10. OLIVER MTUKUDZI, ZIMBABWE
Album 65 zikiwa kwenye tasnia yake ya muziki, katika miaka yake 41 ya muziki, nyimbo zake zimekuwa zikichezwa duniani kote, maarufu zaidi masikioni mwa mashabiki na kibao cha “Neria”
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni