.

Ijumaa, 23 Desemba 2016

Jeshi la Polisi limetangaza magari mapya yaliyoruhusiwa kubeba abiria


Kutokana na mahitaji ya usafiri katika kipindi kuelekea mwisho wa mwaka 2016 pamoja na msimu wa sikukuu, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani na pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini, SUMATRA limetangaza kutoa vibali kwa mabasi aina ya Eicher na Coaster ili kufanya safari za mikoani.
Aidha kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga pia amesema kuwa jeshi hilo limesitisha utendaji wa chama cha kutetea abiria ‘CHAKUA’ mikoani kutokana na kukiuka maadili na kuanzia sasa watabaki na watendaji wa kituo cha mabasi Ubungo pekee.
“Tumeamua kutoa vibali kwenye mabasi mengine ili kurahisisha usafiri kutokana na kuanza kuongezeka kwa abiria, mfano juzi kwenye kituo cha Ubungo yalitoka mabasi 421, jana yametoka mabasi 470 sasa tumeamua kuongeza na Coaster na tumeshafanya ukaguzi mabasi yote yako salama” – Kamanda Mpinga
Download application yetu kwa kubonyeza HAPA

Subscribe katika YouTubechannel yetu kwa kubonyeza HAPA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni