.

Jumamosi, 24 Desemba 2016

Diamond asema ana nyimo alizoimba na Rick Ross, Na Rihana

Wiki chache zilizopita Diamond alitease ujio wa album yake mpya ambayo alisema itakuwa na collabo za kimataifa ikiwemo ya Rick Ross na Rihanna.
Jumatano hii kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, meneja wake, Sallam alifafanua zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa ya collabo hizo.  Sallam amesema collabo na Rick Ross tayari imeshakamilika na ile ya Rihanna ipo kwenye hatua za mwisho, alisema tayari CV na historia ya Diamond imetumwa kwenye uongozi wa staa huyo mkubwa wa Marekani.
Diamond-1
Pia Sallam amesema Diamond ambaye ngoma yake mpya na Neyo ‘Marry You’ imeshaanza kusambaa nchi za nje atatumbuiza atatumbuiza kwenye tuzo CAF 2016, Alhamis ya January 5, 2017 mjini Abuja, Nigeria na pia kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Africa (Total Africa Cup of Nations),itakayofanyika nchini Gabon kuanzia January 14.

Download our smartphone application by clicking here
Subscribe to our YouTube channel by clicking HERE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni