October 4 2016 TANESCO iliwasilisha ombo la kupandisha gharama za umeme kwenye mamlaka ya udhibiti wa nishati, maji na mafuta ‘EWURA’ kwa asilimia 18.19 .
Akizungumza leo December 30 2016 na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa nishati, maji na mafuta ‘EWURA’ Felix Ngamlagosi amesema baada ya EWURA kufanya uchambuzi wake haikuona sababu ya kuongeza kwa asilimia 18.19 badala yake ikapunguza hadi wastani wa asilimia 8.5.
“Pendekezo lao lilikuwa limnalenga kuongeza bei ya umeme kutoka wastani wa sh 242.2 kwa uniti hadi sh 286 kwa uniti, sasa tumepunguza katika makundi yote ya wateja, na tumekataa kuongeza gharama ya asilimia tano kwenye kundi la watumiaji wa uniti chini ya 75 kwa mwezi”
Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520. Bei hizo zitaanza kutumika Januari Mosi mwaka 2017.
TANESCO inatarajia kufanya maboresho ya msongo wa umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu
Bonyeza HAPA kusubscribe katika YouTube channel yetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni