.

Jumanne, 1 Novemba 2016

MKE WANGU ANAWIVU SANA HADI ANAKUWA MWEKUNDU KABISA ASENA MR BLUE



Rapa ambaye amesimama kwenye game la muziki wa Bongo flava kwa miaka mingi sasa, Mr Blue amethibitisha kuwa mke wake anawivu sana hadi anakuwa mwekundu.
Akizungumza hili kwenye FNL, Mr Blue alisema hayo baada ya kuulizwa kuhusu kuwa karibu sana na video queen aliyemtumia kwenye video ya wimbo wa Baki na Mimi kwa kuwa naye karibu sana.
“Mke wangu anawivu vibaya mno hadi anakuwa mwekundu kabisa, Ukiona ivyo inabidi niage kabisa, Ile video ya Baki na mimi, video queen aliye husika ni ndugu na kaka yangu hivyo mke wangu alikuwa anaelewa japokuwa alituma watu kuja kuchungulia nini kinaendele.” Alijibu Mr Blue.
Mbali na hilo, Mr Blue alisema kuwa kwasasa yeye hafanyi tena muziki kama uhuni kwakuwa anazeeka na watoto wake kwa sasa wanakuwa, Hivyo anafanya muziki kama kazi.

Download application yetu HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni