.

Ijumaa, 4 Novemba 2016

Joh Makini atoa neono kwa wanaoanzisha lebo pia ishu ya Lord Eyes



Rapa mkali kutoka Weusi Joh Makini amewachana wanaoanzisha label hapa nchini kuwa wengi wao hawajui vigezo vya kumiliki label na badala yake wanazitumia label kama kiki katika muziki wao.

Joh Makini
Akipiga story ndani ya eNewz amesema, Weusi wana mipango mingi ikiwemo kuanzisha label yao japo wana baadhi ya vijana wanaowasaidia lakini hawa wezi kujitangaza kuwa ni label ya kusaidia wasanii kwa kuwa msaada wanaoutoa ni wa kawaida na sio wakutangaza mitandao.
Hata hivyo Joh hakusita kuelezea mahusiano ya weusi na Lord Eyez
“Lord hajatengwa na bado ni mmoja wa wanafamilia katika kundi letu la Weusi, kuna wimbo wa Lord tulikuwa studio tukiuandaa juzi japo watu wanaongea mengi kuhusu ukaribu wetu na Lord kwa sasa ila siyo mbaya wakituzungumzia kwa kuwa ni sehemu ya maisha yetu”alisema Joh.

Bonyea HAPA kudownload application yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni