.

Alhamisi, 3 Novemba 2016

Black Fox kamapuni iliyokuwa ikifanya kazi na Juliana Isawafo aliyekutwa ameuwawa Arusha yafunguka

Wiki hii katika mitandao ya kijamii kuna picha ambazo zimesambaa zikiuonesha mwili wa msichana anaesadikika kuwa amekufa baada ya kubakwa na watu ambao hawajajulikana na kutupwa nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).
juliana-enzi-za-uhai-wake
Juliana enzi ya uhai wake
Mwili wa msichana huyo ambaye jina lake halisi linadaiwa kuwa ni Juliana Isawafo, ulikutwa katika bonde la mpunga jirani na chuo hicho majira ya saa 5 asubuhi siku ya Jumatano.
Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake halikufahamika mara moja) ameuthibitishia mtandao wa Radio5 Arusha kutokea kwa tukio hilo.
Bongo5 ilimtafuta Mkurugenzi wa kampuni ya Black Fox, kampuni ambayo ilikuwa inafanya kazi na model huyo hapa jijini Dar es salaam.
black-fox
“Juliana sisi tunamjua kama model wa Black Fox na mimi ni managing director,” alisema Mkurugenzi huyo. “Alikuwa ni model lakini pia alikuwa ni dansa Arusha, sisi kuna mtu alitupigia simu akatuambia kuna mtu wenu amefariki, tukawapigia simu ndugu zake kuthibisha tukaambiwa ni kweli. Kwahiyo sisi kama sisi tufanya mkutano ili tupeleke rambirambi kwa ndugu,”
Pia mkurungenzi huyo alisema issue za model huyo kubakwa azitakuja kufafanuliwa na jeshi la polisi likikamilisha upelelezi wake.
“Kwa sasa hivi jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi lakini tunachojua mwili wake umeokotwa jana asubuhi na watu wanadai amekutwa katika hali ambayo anaweza akawa amebakwa. Lakini mimi nadhani vitu kama vivyo tuliachie jeshi la polisi litakuwa na taarifa rasmi kwa sababu wao watajua nini kilitokea.
Pia mkurugenzi huyo alisema watatoa taarifa zaidi ya nini kinaendelea pamoja na kutangaza nini wameandaa kwa ajili ya kuwapa pole wafiwa.
Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema Juliana hakuwahi kufanya kazi na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza katika mitandao.
Katika mitandao ya kijamii Alhamisi hii kulizuka uvumi usio wa kweli kuwa model huyo aliyefariki ni yule aliyeonekana katika video ya wimbo Salome wa Diamond Platnumz.

Bonyeza HAPA chini kudownload application yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni