.

Jumatatu, 14 Novemba 2016

Alicia Keys azungumzia kuishi bila kujipaka vipodozi

Mwimbaji kutoka Marekani Alicia Keysamefunguka kuhusu kujiamini kwake kutembea kwenye shughuli kubwa za muziki bila kujipaka vipodozi usoni mwake.
Alicia Keys amesema ilichukua muda mrefu sana kusafisha ngozi yake ili kuweza kukaa mbele za watu bila kipodozi chochote usoni mwake.
Keys anasema siri yake ilikuwa kupunguza mafuta na cream alizokuwa akinywa kabla hanajapa ujauzito na akazidisha kiasi cha maji anachokunywa kwa siku ndio maana ngozi yake ikawa safi.
Kwa sasa Alicia Keys anatembea bila kujipaka kipodozi chochote kwenye#RedCarpet na hata kwenye kiti chake cha ujaji wa shindano la vipaji la #The Voice.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni