.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

Volkswagen kuwalipa faini kwa wamiliki


Hakimu wa mahakama kuu nchini Marekani ameidhinisha faini ya karibu dola bilioni kumi na tano kwa ajili ya madai dhidi ya kampuni ya kutengeneza magari Volkswagen ya Ujerumani juu ya kashfa ya uzalishaji wake wa dizeli.
Wamiliki Karibu nusu milioni wa Volkswagen wataweza kurudisha magari yao au kufanyiwa marekebisho, Pia watapokea fidia ya hadi dola elfu kumi.
Volkswagen ilikiri mwaka jana kuwa ilifanya udanganyifu juu ya majaribio ya uzalishaji wa dizeli ili kufanya magari yake kuonekana safi.
Hukumu hiyo ni rekodi kwa ajili ya sekta ya magari nchini Marekani, lakini Volkswagen inakabiliwa na gharama zaidi, kwa faini na kesi za kisheria kutoka majimbo kumi na sita nchini Marekani na katika nchi nyingine.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni