.

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

India yaanzisha app kwa ajili ua kilimo

Tumeshazoea kuona taxi za Uber zikirahisisha usafiri kwa abiria wa jiji la Dar es Salaam – sasa kampuni ya kutengeneza magari ya Mahindra and Mahindra ya nchini India imeanzisha App mpya itakayotoa huduma ya matrekta kwa ajili ya kulimia.
_91982940_5856309e-247c-4bbd-9cca-dfcb4bab078f
App hiyo iliyopewa jina la Trringo itawarahisishia wakulima wa jimbo la Karnataka kuweza kupata urahisi wa kulima kwa kutumia kilimo cha trekta huku huduma hiyo ikitarajiwa kupatikana kwa kiasi cha dola 6 kwa saa moja.
Afisa Mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Rajesh Jejurikar ameliuambia gazeti la New York Times kuwa wameleta mpango huo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa nchi hiyo huku huduma hiyo ikitarajiwa kupatikana kwenye majimbo ya Gujarat, Madhya Pradesh na Maharashtra kwa hapo baadaye.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa kwa sasa huduma hiyo itakuwa inapatikana kwenye vituo 20 vya jimbo la Karnataka lakini pia wakulima watakao hitaji huduma hiyo watakuwa na uwezo wa kupiga simu za moja kwa moja kwenye maeneo ambayo hayana huduma ya internet.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni