Moja ya vitu ambavyo vinatrend kwa sasa ni kuhusu kitabu cha Biblia alichokuwa anatumia 2pac wakati upo jela kimetajwa kuuzwa kwa $54,000 sawa na milioni mia na ushwee
Mtandao wa Moments In Time unaojishughulisha na maswala ya autograph unatarajia kuuza Bibliailiyokuwa inatumiwa na 2Pac wakati yupo jela baada ya kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji mwaka 1995, Biblia hiyo ambayo inaonyesha saini ya 2pac pamoja na namba ambayo alikuwa akiitumia huko kifungoni 95A1140.
Februari 15 Mwaka 1995 ndio siku ambayo Tupac alianza kutumikia kifungo chake baada ya kukutwa na mashitaka ya ubakaji, lakini wakati akiwa anatumikia kifungo chake pac aliwahi kuachia Albamu yake ya Me Against The World na kumfanya kuwa msanii wa kwanza Album yake kushika namba moja katika chati za Billboard 200.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni