.

Jumatano, 14 Septemba 2016

TIDAL YA JAY Z YAPATA HASARA YA DOLA MILIONI $28


Siku zote pale ambapo umewekeza ili upate mafanikio daima lazima kutakuwa na matatizo ambayo nayo yatakuwa kama njia ya kukuboost.
Mtandao wa Tidal wa kustream ngoma online waJay z umeripotiwa kupata hasara ya dola milioni 28,The Wall streat Journal imeripoti jana kwamba kampuni ambayo inasimama kama Baba wa Tidal, Aspiro imepata hasara ya mkwanja huo japokuwa kampuni hiyo ni kubwa na inamiliki wasanii wakubwa na vilevile ikiwa inamashabiki milioni ambao wanaufuata huo mtandao.
Jay z aliununua huo mtandao mwaka jana mwezi wa tatu kwa mtonyo wa dola milioni 56, katika kipindi cha mwezi huohuo Jay z pia aliwaunganisha marafiki zake ambao nao ni wasanii wakubwa kwenye industry yake huku akiwa na kauli ya kwamba mtandao huo utakuwa unawaingizia wasanii pesa kwenye mifuko yao bila tabu.
Maybe time itakuwa imefika labda Jay anaweza kukubali kuungana na kampuni ya Apple kuinua zaidi Tidal, kutokana na Apple Music kujibebea umaarufu kwa kuifanikisha Album ya Drake Views kupata chati kubwa na mafanikio kibao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni