.

Ijumaa, 9 Septemba 2016

Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo September 9 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September  09 2016 amemteua Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.
Aidha Rais Magufuli amemteua Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni