Kupitia taarifa zilizotolewa kutoka Spain zimeripoti kwamba ndege hiyo binafsi ya Cristiano Ronaldo imepata ajali katika uwanja wa ndege wa Barcelona’s El Prat baada ya gia ya kutua kuharibika ghafla na kushindwa kutua vizuri.
Good Newz ni kwamba Cristiano Ronaldo hakuwepo ndani ya ndege hiyo na rubani wa ndege hiyo pia alipata huduma ya kwanza baada ya kupata majeraha madogo madogo.
Ndege hiyo inayofahamika kutoka katika kampuni ya Gulfstream G200 twin-engine, ni ndege ambayo Cristian Ronaldo alinunua kwa gharama ya €19 milioni ikiwa na mabafu ya wafanyakazi pamoja na abiria, huduma ya internet, friji pamoja na DVD player.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni