.

Jumanne, 13 Septemba 2016

Mr Blue asema hawezi kurudia matapishi


Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Mboga Saba’ amefunguka na kusema kuwa saizi yeye ni mtu mzima anaangalia maisha yake na familia yake hivyo hawezi kurudia matapishi ambayo tayari alishakwisha yatapika.
Mr Blue alisema haya kupitia eNewz alipokuwa akifafanua juu ya taarifa zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa alimpigia simu aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Naj ndipo hapo aliposema hawezi kurudia matapishi aliyokwisha yatapika.
“Niliongea na Baraka The Prince alisema kuwa wao hawakufanya hilo jambo, lakini kama wangekuwa ni wao lazima ningetafuta njia ya kuwashikisha adabu maana huko ni kuharibiana.

Mimi saizi nimeshakuwa mtu mzima siwezi
kurudia matapishi ambayo nilishakwisha yatapika mwanzo’ alimalizia Mr Blue.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni