.

Jumapili, 25 Septemba 2016

Jumba la makumbusho la Wamarekani Weusi lafunguliwa na Barack Obama

Rais wa Marekani Barrack Obama amefungua rasmi jumba la kumbukumbu za Wamarekani-weusi mjini Washington DC.
Obama amesema kuwa jumba hilo la utamaduni na historia ya Wamarekani weusi litatoa historia ya Marekani ambayo haijatambuliwa na wengi.
Mtindo wa Jumba hilo ulichorwa na raia wa Uingereza David Adjaye.
Huku baadhi ya vitu vilivyopo katika jumba hilo vikionyesha wakati wa utumwa, vyengine vinaonyesha utamaduni wa watu weusi ambao umeingia katika utamaduni wa Marekani.
Wanaharakati wa haki za watu weusi nchini Marekani walipendekeza kujengwa kwa jumba hilo mwaka 1915.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni