.

Jumatatu, 26 Septemba 2016

Japan yarusha ndege zake juu ya visiwa vya China

Japan imesema kuwa ilirusha ndege zake hewani siku ya Jumapili baada ya ndege nane za China kupaa kati ya visiwa vya vyake.
Ndege hizo zinaozodaiwa kuwa zile za kurusha mabomu,kufanya uchunguzi pamoja na ndege ya kivita ,zilipaa juu ya Miyako,kati ya Okinawa na Miyakojima.
China imesema kuwa takriban ndege 40 zilihusika katika kile inachokitaja kuwa zoezi la kawaida.
Ndege hizo hazikupita katika anga ya Japan,lakini hatua hiyo inaonekana kuwa maonyesho ya ubabe ya China.
Ramani ya visiwa vya Japan ambayo ndege ya China ilipita juu yake
Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Japan kusema itashiriki katika zoezi la pamoja na wanamaji wa Marekani katika bahari ya kusini mwa China.
Msemaji mkuu wa Japan amesema kuwa taifa hilo linachunguza hatua hizo za China kwa karibu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni