Tujikumbushe..
Mwaka jana Diamond alishinda kipengele hiki na akashindana kipengele kimoja cha ‘Best Worldwide Act: Africa/India’ na mshindi wa Best Indian Act ambaye mwaka jana alikuwa ni muigizaji na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi pia kuwa Miss World mwaka 2000.
Priyanka ambaye kwa sasa ni muigizaji wa tamthilia mpya ya Marekani, Quantico inayorushwa na kituo cha ABC.
Kura yako nimuhimu sana kumuwezesha Alikiba kufikia level kama hii.
Mchongo huu hapa..
Alikiba ametajwa kuwania kwenye tuzo za mwaka huu za MTV Europe Music Awards (EMA) kipengele cha Best African Act.
Anakuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kutajwa kuwania kipengele hicho.
Kiba atachuana na wasanii wengine wakiwemo Wizkid na Olamide wa Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.
Kama ilivyokuwa mwaka jana, mshindi katika hatua ya kwanza ataendelea kwenda kuwania kipengele cha Worldwide Act: Africa/India ambacho mwaka jana alishinda Diamond Platnumz.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni