.

Jumanne, 2 Agosti 2016

SHAMSA FORD AMTAMBULISHA MPENZI WAKE MPYA

Sahau kabisa kuhusu msanii Nay wa Mitego juu ya kutoka kimapenzi na Mwanadada mrembo kutoka Bongo Movie Shamsa Ford.
Weekend iliyopita ilikuwa ni Birthday ya mwanadada Shamsa Ford, na Birthday Party ya mwanadada huyo ilifanyika Club Bilcanas usiku wa Jumapili ya tarehe 31 July, ndipo mwanadada huyo alipo chukua nafasi ya kumtambulisha rasmi mpenzi wake ambaye anafahamika kama Chddy Mapenzimfanya biashara maarufu wa nguo jijini Dar es Salaam.
Kabla ya Shamsa Ford kuchukua uamuzi huo wa kumuonyesha hadharani mpenzi wake huyo alikuwa akiwaacha watu midomo wazi katika mitandao ya kijamii baada ya kuwa ana post picha au video akiwa na mpenzi wake huyo lakini bila kumuonyesha sura. Jambo ambalo lilikuwa linawatatiza watu wengi kwa kuwa na shauku ya kutaka kumjua mwanaume huyo aliyekuwa akipostiwa na Shamsa Ford.
“Mwanzo nilikuwa naficha kwasababu ya uoga na vitu kama hivyo lakini mapenzi yakikuzidi mwisho wa siku unashindwa kujizuia, utajikuta tu unajionyesha” Alisema Shamsa Ford wakati akihojiwa na E-News ya EATV.
Shamsa Ford pia aliweka wazi kuwa tayari Chiddy Mapenzi ni mtu ambaye anafahamika mpaka nyumbani kwao na tayari wamekwisha fanya hadi taratibu za MAHARI.
Shamsa Ford pia ameweka wazi kuwa anataka kujikita rasmi katika biashara ya nguo, Biashara ambayo anaifanya mpenzi wake huyo wa sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni