.

Jumanne, 2 Agosti 2016

BABU TALE AFIKISHWA MAHAKAMA KUU KWA KOSA HILI


Baada ya kushindwa kulipa fidia ya milioni 750 aliypoewa kama adhabu na mahakama kwa  kuvunja sheria ya hakimiliki, Babu tale amejikuta akifikishwa kwenye mikono ya mahakama kwa kugoma kufungwa kwa kushindwa kulipa fidia hiyo
Meneja wa Diamond platnumz, Hamisi tale a.k.a Babu tale, leo inaweza kuwa ni siku mbaya kwake kutokana na kushikiliwa na Mahama Kuu Kanda ya Dar es salaam ili atoe maelezo ni kwanini hataki kufungwa kwa kushindwa kutekeleza agizo la Mahakama la kumlipa fidia Shekhe Mbonde shilingi milioni 750.
Tukio hilo limetokea pale Babu tale alipochukua hatua za kuuza nakala za CD za Mawaidha ya Shekhe Mbonde bila idhini yake ambapo kwa sheria za nchini ni kosa.
Shekhe Mbonde alifungua Madai hayo kwa kuishitaki kampuni ya TipTop Connection ambayo inasimamiwa na Babu tale kwa kusambaza nakala hizo. Sasa Sheikh Mbende alihitajika kulipwa fedha shilingi milioni 700 kwa faida ambayo aliitegemea kuipata kupitia CD hizo na kwa kuvunja hakimiliki.
Kingine Mahakama ilitaka alipe shilingi milioni 50 kama damages na vilevile kufungiwa kutojihusisha kwa muzo yoyote na kusambaza kazi za Sheikh Mbonda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni