.

Jumatatu, 29 Agosti 2016

Serikali yavifungia vituo viwili vya radio kwa makosa ya uchochezi


Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.

Lakini pia Waziri Nape amesema huku adhabu hiyo ikianza leo August 29 2016 pia ameiagiza kamati yake kuviita vyombo hivyo kwa ajili ya kuzungumza navyo kisha maamuzi mengine ya kisheria yatachukuliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni