Muogeleaji wa Marekani Ryan Lochte amepoteza mikataba yake yote minne ya udhamini baada ya wenzake watatu kudanganya kuwa waliibiwa na wezi waliokuwa na silaha katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika mjini Rio.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa muogeleaji huyo anaweza kutokushiriki kabisa mashindano mengine ya kuogelea.
Kampuni ya uogeleaji ya Speedo ilikuwa ya kwanza kusitisha mkataba wake ikifuatiwa na Luxury retailer, Ralph Lauren, The Skin Care company,na Kampuni ya matress na Airweave.
Lochte bado anakabiliwa na mashitaka ya kujibu kwa mamlaka ya michezo nchini Brazil ikiwa ni uhalifu pamoja na utovu wa nidhamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni