.

Jumamosi, 13 Agosti 2016

HAKUNA TENA KWENDA JELA, TYGA AMEKAMILISHA DENI LAKE



Baada ya kuandamwa na kibali cha kukamatwa kushindwa kulipa deni na kutofika mahakamani,Tyga amekamilisha pesa yote anayodaiwa.
Ishu nzima ilianza siku ya jumanne August 9 ambapo rapper Tyga alishindwa kufika Mahakamani kujibu mashitaka ya kwanini ameshindwa kumlipa mwenye nyumba wake pesa za kodi ambazo ni$480,285 alikuwa anadaiwa, mpango mzima wa kulipa deni hilo umekamilishwa jana kwa taarifa kutoka People Magazine.
Haijafahamika ni kiasi gani ambacho Tyga amelipa, ila kupitia mtandao wa Tmz umesema kwamba Tyga amelipa pesa yote aliyokuwa anadaiwa ambayo ni $480k ukijumlisha na zile zingine za uharibifu alioufanya kwenye mjengo huo ambao uko Malibu.
Taarifa zingine zinasema kwamba tayari mwenye nyumba huyo ameshaenda kuonana jaji kwa ajili ya kufuta kibali cha kukamatwa kwa Tyga kutokana na Pande zote mbili kumalizana vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni