.

Alhamisi, 4 Agosti 2016

CHRIS BROWN AKUMBANA NA KESI NYINGINE YA KUMPIGA MTU RISASI


Huu mwaka umekuwa ni mmbaya kwa mnyamwezi Chris Brown, Chris brown amefunguliwa mashitaka ya kumuumiza jamaa kwa risasi ndani ya klabu.
Tukirudi nyuma mwaka 2014 mwezi wa sita, moja ya mtu muhimu sana kwenye industry ya muziki, CEO wa Death raw records Suge Knight alimshitaki Chriis brown baada ya kupigwa risasi sita katika pre party show ya VMA iliyokuwa hosted na Chris brown.
Sasa Kwa mujibu wa Tmz, muathirika wa risasi mwingine amefata nyayo za Suge Knight kwa kumfungulia kesi Chris Brown kwa kudai kuwa anawajibika kwa majeraha yake.
Muathirika huyo wa risasi anayejulikana kama Ginja Elms, anasema kuwa kwenye klabu hiyo aliyopigwa risasi watu walikuwa wanafahamu Chris Brown alivyokuwa karibu na makundi ya uhalifu ndani ya klabu hiyo na walinzi wa klabu hiyo pia hawakuchukua jukumu la kumkagua kila mtu aliyekuwa anaingia katika ukumbi huo.
Ginja Elms bado anatafuta zaidi ya dola $750,000 kwa Chris Brown na Pia Mia kama majeraha ya mwili aliyoyapata na kwa usumbufu alioupata kwenye mahusiano yake na mkewake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni