.

Jumapili, 17 Julai 2016

Sudan Kusini yakataa majeshi zaidi


Serikali ya Sudan Kusini imekataa kata kata pendekezo la viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki la kuongeza wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini humo.

Viongozi wa ukanda huo chini ya mwamvuli wa Mamlaka ya kusimamia maendelea IGAD na umoja wa mataifa walikuwa wamependekeza hatua 7 za kuthibiti hali ya usalama nchini Sudan Kusini na kuizuia taifa hilo changa zaidi kutotumbukia katika lindi la mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Majuzi zaidi ya watu 300 wengi wao wakiwa ni wanajeshi walipoteza maisha yao uhasama baina ya wanajeshi watiifu kwa makamu wa rais Riek Machar walipokabiliana na wale wanaomuunga mkono rais Salva Kiir katika mji mkuu wa Juba.

Umoja wa mataifa unasema kuwa watu takriban elfu 40 walilazimika kuhama makwao kufuatia mapigano hayo.
Sasa balozi wa Sudan Kusini katika Umoja wa Afrika James Pitia Morgan ameiambia BBC kuwa Sudan Kusini kamwe haitoruhusu askari yeyote yule kuingia nchini humo.

Bwana Morgan amesema haina maana kwani tayari kikosi cha walinda amani wa umoja wa mataifa UNMISS kina zaidi ya askari 12,000.

Kikosi hicho cha UNMISS kinalaumiwa na viongozi wa IGAD kwa kushindwa kuwalinda raia moja ya malengo kuu ya kuwepo kwao huko.

Viongozi wengine akiwemo rais wa Uganda Yoweri Museveni wamepinga pendekezo la katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki Moon ya taifa hilo kuwekewa vikwazo dhidi ya ununuzi wa silaha .

Mapendekezo hayo ni miongoni mwa mengine 6 ambayo yanatarajiwa kuratibiwa na umoja wa mataifa ya Ulaya AU inayoendelea mjini Kigali Rwanda.

Mkutano huo wa viongozi wa muungano wa Afrika unaanza leo Jumapili na kumalizika Jumatatu nchini Rwanda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni