Morroco imetoa tamko la nia yake ya kutaka kujiunga tena katika umoja wa Afrika.
Katika ujumbe ulitumwa kutoka kwenye mkutano wa Umoja wa Matataifa nchini Rwanda,mjini Kigali,Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita amesema sasa ni wakati muafaka kwa taifa lake kurejea na kuchukua nafasi yake katika jumuiya hiyo ya umoja wa Afrika.
Morocco ilijitoa katika umoja huo mwaka 1984 wakati umoja huo ulipotambua uhuru wa eneo la magharibi mwa sahara.
Ambapo Morocco ilidai kuwa eneo la magharibi mwa sahara lilikuwa ndani ya mipaka yake.
Hata hivyo Umoja wa Afrika umesema utaendelea kusukuma upatikanaji wa haki ya watu wa eneo la Magharibi mwa Sahara ili kuwa na uhuru kamili bila kuingiliwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni