.

Jumanne, 19 Julai 2016

Melania asema mumewe Trump ataifaa Marekani

Mkewe Donald Trump, Melania, ameuambia mkutano wa kitaifa wa chama cha Republican kwamba mumewe ni mshindi ambaye hawezi kuivunja moyo Marekani.

Mwanamitindo huyo wa zamani aliyezaliwa Slovenia, alikuwa mzungumzaji mkuu katika siku ya kwanza ya kikao hicho mjini Cleveland.

Awali kulikuwa na ghasia wakati wajumbe walipopiga kelele na kuzomea kukataliwa ruhusa kudhihirisha upinzani wao kwa Trump kuwa mgombea.

Melania Trump, ameuambia mkutano huo kwamba mumewe ni mshindi ambaye hawezi kuiangusha Marekani.

Mwanamitindo huyo wa zamani aliyezaliwa Slovenia, alikuwa mzungumzaji mkuu katika siku ya kwanza ya kikao hicho mjini Cleveland.

"Iwapo mnataka mtu awapiganie na apiganie nchi yenu, naweza kuwahakikishia huyu ndiye munayemhitaji.

Hawezi katu kukata tamaa na muhimu zaidi hawezi kuwaaibisha,” amesema.

Awali kulikuwa na ghasia wakati wajumbe walipopiga kelele na kuzomea kukataliwa ruhusa kudhihirisha upinzani wao kwa Trump kuwa mgombea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni