Msanii wa Bongo Fleva anaye fanya kazi chini ya lebo ya Tiptop Connection Madee amesema kwamba adhabu zinazotolewa na BASATA hazitoshi kuwa fundisho kwa wasanii na kuwafanya wasirudie makosa kwa sababu haoni kama zina madhara kwa wasanii.
Akiwa ni mmoja kati ya wasanii ambao wameshawahi kuzipitia adhabu hizo za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ameyazungumza hayo baada ya kuona baadhi ya wasanii kurudia makosa hata kama wamewahi kufungiwa na baraza hilo.
“Swala la BASATA mi naona bado adhabu zao hazijawa timilifu, adhabu zao haziwezi kumuathiri mwanamuziki yeyote kwasasa labda kama wakiamua kubuni kitu kingine ili kifanyike.
Kwasababu unapoamua kuifungia nyimbo wakati nyimbo inakuwa tayari imeshatoka na kusambaa mitandaoni kote halafu wewe unasema umesha ifungia inakuwa too late, kwasababu huwezi kumzuia mtu kusikiliza nyimbo nyumbani kwake hata kama wewe BASATA umeifungia.” Alisema Madee.
Hakuishia hapo raisi huyo wa Manzese kama anavyo jiita aliendelea kuongeza kuwa “Mtu haathiriki na chochote sana sana unakuwa umemkikisha tu kwasababu unaposema nyimbo imefungiwa mtaani ndio wataanza kukuzungumzia kwahivyo nyimbo inazidi kuongelewa na inazidi kufanya poa tu kwenye mitandao.” Aliongeza Madee
Madee alitoa wazo kwa BASATA kuwa waongeze adhabu kwasababu msanii akipewa adhabu ikimuathiri ataogopa kurudia tena kosa ambalo amelifanya mwanzo.
Madee ni Msanii ambaye amewahi kuathiriwa na adhabu za BASATA kwa mujibu wake kuwa ilimsababishia kushindwa kupewa tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kwasababu nyimbo ile aliyodhani ilistahili kupewa tuzo haikuwa na maadili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni