.

Jumapili, 17 Julai 2016

Drake ameamua kujibu Disstrack za Joe Budden kwenye ngoma ya “No shopping”


Lile bifu zito lililopo kati ya Rapper Drake na JoeBudden linazidi kuchanua, Baada ya Joe Budden kuachia diss track tatu kwenda kwa Drake, Drake naye ametumia nafasi ya kumjibu Budden kwenye ngoma aliyoshirikishwa na French Montana inaitwa “No shopping”.

Bifu la Drake na Budden lilianza pale rapper kutoka Torronto, alipoachia ngoma yake ya “4pm in Calabasas” ambayo ilikuwa ikumuhusu jamaa yake Budden kwamba ni mtu ambaye huwa anategemea washikaji wamlipie wanapokuwa out. Ngoma hiyo ilimfanya Joe Budden kuamka na kutoa Disstrack tatu ambazo zilikuwa zimebeba ujumbe mzito kwa Drake.

Kama unavyojua, Drake ni moja ya wasanii ambao huwa sio mtu wa haraka kukurudishia Disstrack lakini anapoamua kuibuka na kukujibu lazima mashabiki wanyooshe mikono juu kutokana na uwezo wake mistari anapokuwa anaandaa ngoma, Drake amemjibu Joe Budden bila kuficha kwenye ngoma ya No shopping aliyoshirikishwa na French Montana.

“Pump, pump, pump it up, she got a good head on her, but I pump it up / I’m not a one-hit wonder, they know all my stuff / You let me turn into the nigga that you almost was, I done seen a lot of shit and I done been in things, and I never started nothin’, I just finish things / And I’m still off like the man that brought me in this thing, how you out here celebratin’ like the winnin’ team?” Alisema Drake kwenye ngoma ya No shopping.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni