.

Jumatano, 8 Juni 2016

Mambo Muhimu Kuhusu Antivirus /Internet Security katika computer zetu


Karibu mpenz msomaji katika makala hii ya leo hapa. leo naenda kuwaletea mambo muhimu kuhusu hizi antivirus na internet security katika computer zetu.

Watumiaji wengi haswa watumiaji wa tarakishi ( computer/simu ) wanatumia vifaa vyao hivyo na kuingiza ( install ) programu za kulinda vifaa hivyo dhidi ya virus na mashambulizi mengine kwa njia ya mtandao kama kifaa hicho kimeunganishwa na mtandao .

JE ANTIVIRUS NI NINI
Antivirus ni programu inayowekwa katika tarakishi ( computer/simu ) kwa nia ya kulinda tarakishi hiyo dhidi ya virus na ambao wanaweza kusambaa na kuhamishwa kwa njia nyingi tu .

INTERNET SECURITY NI NINI ?
Internet Security ina tabia na mambo mengi kama antivirus lakini hii imeongezewa zaidi na kwa wale wanaotumia mtandao ni vizuri kuwa na Internet Security kuliko Antivirus .

Tofauti kubwa kati ya Internet Security na Antivirus ni hiyo Firewall , lakini sio zote ziko hivyo .

AINA/MAKUNDI YA ANTIVIRUS
Kuna Makundi mengi ya antivirus kutegemeana na aina ambazo mtu anataka kwa ajili ya shuguli zake za kila siku .
Antivirus Huria /Bure (Free )
Hizi ni Antivirus ambazo unaweza kushusha ( download ) toka kwenye mtandao na kuzitumia kwa ajili ya ulinzi wa tarakishi yako lakini huwa zinakosa baadhi ya vitu au baadhi ya vitu vimefungwa mfano wa Programu hizi ni AVG 2014 , AVAST 9.0 ,Kaspersky .

Utaona kwamba unatakiwa kusajili AVAST ndani ya siku 30 au itaacha kufanya kazi , AVG haikulazimishi ila haina Firewall Kaspersky nayo inasiku 30 baada ya hapo itazima usipoweka Leseni .

Trial/Demo ( Majaribio )
Antivirus hizi ni Bure kabisa na zinaweza kupatikana kwenye tovuti kadhaa lakini matatizo yake ni kwamba zenyewe ni za muda fulani baada ya muda huo zinajifunga hazitoweza kufanya kazi mpaka ununue leseni yake kwa njia ya mtandao kampuni zinazotoa antivirus za majaribio ni kama Symantec yenye Norton Antivirus na Kaspersky .

Full Version /Licensed /Za Kununua
Mara nyingi mtaani watu wanaita za kununua kwa sababu unakuwa unapata kila kitu na kama unahitaji Keys au Leseni yake unaweza kuiona imeandikwa au iko ndani ya CD yenye Programu hiyo au kama umenunua kwa njia ya mtandao basi utatumiwa kila kitu kwenye Anuani ya Barua pepe yako na maelezo ya kutosha .

Cha muhimu kujua ni kwamba ubora wa antivirus hautegemei na bei ya antivirus uliyonunua au aina ya antivirus uliyonunua mara nyingi inategemea hata mazingira unayofanyia kazi na aina za kazi unazofanya na mambo mengi zaidi .

Ni vizuri ukanunua antivirus na kuwa na leseni yake ili siku nyingine uweze kutumia leseni hiyo kama limetokea tatizo kwenye tarakishi yako na kuamua kufuta vitu .

VIRUS WANASAMBAA KWA NJIA GANI
Kuna njia kuu 2 ambazo zinaweza kusambaza Virus
Moja ni kwa kutumia vichomekwa kama Flashdisk , hii mara nyingi inatokea pale mtu anapoingiza flashdisk yake kwenye tarakishi iliyoadhirika na virus .

Mbili ni kwa njia ya mtandao hii inatokea pale mtu anaposhusha ( download) viru kutoka kwenye mtandao kama ni programu ambayo inaweza kuwa na virus ( hii inategemeana na chanzo cha programu hiyo ) au faili ambalo anaweza kuwa ametumiwa na mtu .

Njia nyingine zilizobaki hazitumiwi sana na wahalifu na kama zikitumiwa basi huwa na malengo fulani haswa yanayohusiana na ujasusi na aina nyingine za uharamia kwa njia ya mtandao .

MAISHA YA ANTIVIRUS
Maisha ya Antivirus yanaanza pale unapoingiza kwenye tarakishi yao au vifaa vingine vya mawasiliano kama simu ya mkono .

Maisha ya antivirus mara nyingi ni muda wa mwaka mmoja lakini inategemeana na leseni uliyonunua kwenye bidhaa husika wengine wanatoa hata miaka 2 kwahiyo ni kuanzia siku uliyoweka mpaka mwaka siku zaidi ya 300 ziishe .

Jambo muhimu kuliko zote kujua ni kwamba pale unapoingiza antivirus kwenye tarakishi yako inakuwa tayari imeshapitwa na wakati ( outdated ) na nguvu yake inakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa sana unatakiwa uweke updates ili iweze kwenda na wakati na kuwa imara .

Watu wengi wanapenda kuweka antivirus kwenye tarakishi zao na programu nyingine bila kuziboresha zaidi ( kufanya updates ) matokeo yake ni kwa programu hizo au antivirus hizo kufanya kazi chini ya kiwango na kushindwa kupambana na virus na matishio mengine yaliyopo kwenye ulimwengu wa tarakishi haswa kwa njia ya mtandao .

MWISHO WA ANTIVIRUS .
Mwisho wake ni pale mtu anapochoka kutumia bidhaa hiyo na kuamua kutumia bidhaa nyingine anaamua kuiondoa kwenye tarakishi yake , kama imefikia hivyo unaweza kutumia njia ya ADD/REMOVE PROGRAMES au UNINSTALL au unaweza kutafuta programu maalumu ya kuondolea programu hiyo .

Kwa sasa kampuni nyingi zinazotengeneza antivirus zina programu maalumu kwa ajili ya kuondolea bidhaa zao kwenye tarakishi unaweza kupata bure programu hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni