.

Ijumaa, 24 Juni 2016

CONFIRMED: Mkenya Wanyama amejiunga na Tottenham Hotspurs

Baada ya kiungo wa kimataifa wa Kenya na nahodha wa Harambee Stars aliyekuwa anaichezea klabu ya Southampton ya England Victor Wanyama mwenye umri wa miaka 24 kuhusishwa kwa muda mrefu kutaka  kujiunga na Tottenham Hotspurs, jana June 23 amemaliza rasmi uvumi huo.

Wanyama ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga na Tottenham Hotspurs kwa zaidi ya wiki mbili, amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Tottenham Hotspurs, kwa ada ya uhamisho ambayo ni siri pande zote mbili hawajaweka wazi.
mawa
Wanyama alikuwa akitajwa atajiunga na Tottenham Hotspurs kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 11, ambazo ni zaidi ya bilioni 35 za kitanzania. Taarifa hizo zinakuwa njema kwa Afrika Mashariki, kwani staa huyo pekee Afrika Mashariki katika Ligi Kuu England atapata nafasi ya kucheza UEFA Champions League msimu ujao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni