.

Jumatano, 8 Juni 2016

CONFIRMED: Man United imemsajili Eric Bailly leo June 8 2016

Klabu ya Manchester United ya Uingereza leo June 8 2016 imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea klabu ya Villarreal  yaHispania Eric Bertrand Bailly.

Man United imefanikiwa kumsajili Eric Bertrand Bailly kwa mkataba wa miaka minne, mkataba ambao una kipengele cha kumuongezea miaka miwili zaidi, Eric Baillyalijiunga na Villarreal January 29 2015 na ameichezea jumla ya mechi 47 na mechi 15 kaichezea timu yake ya taifa ya Ivory Coast.
CCBB26E85052403E8BC4AEC5AE6C0562
Bailly mwenye umri wa miaka 22 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Ivory Coastwaliofanikiwa kutwaa Kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2015 na alicheza jumla ya mechi zote sita za mashindano hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni