.

Alhamisi, 9 Juni 2016

Chuo kikuu chawalipa wahalifu wa mtandao Canada


Chuo kimoja kikuu nchini Canada kimewalipa wahalifu wa mitandaoni kurudisha data walioibadilisha na kuwa kitu kisichoeleweka.

Chuo kikuu cha Calgary kililazimika kuwatumia wahalifu hao takriban dola 20,000 za Canada baada ya kushindwa kurekebisha uharibifu uliofanywa na kirusi kwa jina ransomware.

Kirusi hicho hufanya ujumbe na faili nyengine kutosomeka.

Mtaalam mmoja ameonya kuwa malipo hayo yatawashinikiza wahalifu wengine kufanya utapeli kama huo.

Hatua hiyo inajiri wiki ambapo kampuni ya Intel ilionya kuwa kirusi hicho cha ransomware kilikuwa kikienea kwa kasi ya juu.

Kuna zaidi ya virusi 120 vya kompyuta,vingi huimarishwa na hivyobasi huwa vigumu kwa wataalam wa usalama wa mtandaoni kutoa suluhisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni