.

Alhamisi, 30 Juni 2016

Breaking news: Mh Joseph Mbilinyi(Sugu) amesimamishwa kuhudhuria vikao 10 vya Bunge


Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya Hiphop na Hit maker wa ngoma ya Freedom ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho.

Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo.

 Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni