Moja ya story kubwa June 02 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘Kina Zitto , Lissu, Mdee kukatwa mshahara, posho’, gazeti hilo limeripoti kuwa wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.
Gazeti hilo limesema wabunge hao ambao jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe, Tundu Lissu,Halima Mdee, Ester Bulaya, John Heche naGodbless Lema.
Gazeti hilo limeongeza kuwa adhabu hiyo iliyotolewa kama azimio la bunge baada ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na kuomba muongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi
Habari zilizopatikana bungeni na kuripotiwa na Gazeti hilo la Mwananchi zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na kanuni ya bunge ya 75 ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa kazi’. Akizungumzia na gazeti hilo Zitto alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa barua inayoeleza mambo hayo wala kusimamishwa bunge.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni