.

Jumanne, 24 Mei 2016

Wema azindua application yake ya Simu “Wema Sepetu mobile application”

Mwenyewe anasema ‘This May won’t be the same’ Wema Sepetu amezindua application yake mwnyewe ya simu “Wema Sepetu mobile application”

Wema Sepetu alisema amefungua application yake ilikuwaweka mashabiki wake karibu yake.
“Kwanza Kabisa nichukue nafasi hii Kusema Asante Mungu wangu kwa kunifanikisha kukamilisha kile ambacho nimekuwa nikikitamani na ambacho nimefanyia kazi kwa takribani ya miezi Mitano mpaka kufika siku hii ya leo…” Wema ameandika kwenye Instagram yake “Lakini pia niseme Asante kwa Familia yangu yote kwa ujumla, Bila kusahau mashabiki wangu wapenzi kwa kunipa moyo wa kutokukata tamaa japokuwa kuna mengi ambayo kwa binadamu wa kawaida huwezi vumilia Ila kiukweli mashabiki wangu mmekuwa mnanipa nguvu na Courage everyday…”
“Najisikia Fahari sana Leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Barani Africa Kuwa na MobileApp inayonitangaza mimi Mwenyewe kama Content….” Alielezea “Kwa kutumia hii App unaweza kupata chance ya kupata zile habari zote za uhakika kuhusu Wema Sepetu… Kuna vingi ambavyo pia unaweza kupata kama Video Clips, Audio na Pictures kwa wale watumiaji wa Smart Phone… Lakini pia kwa wale wasio na Smart phone basi unapata Habari na Matukio mbali mbali kuhusu mimi ambayo sio Longo longo… Trust me with this app kuna mengi saaana mtakayoyapata… Ni Rahisi sana Una tuma Neno “Wema” kwenda namba 15404 and u are done…. Asanteni sana…. Nawapenda Mno… Huduma hii ipo Applicable kwa Mitandao Yote Tanzania…. What are u waiting for…? “
Wema alifanya mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuzindua application hiyo, Mh, Nape Nahuye alihudhulia uzinduzi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni