“10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHAZ ya hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwaCrocodile House.
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwaShoe House, iko South Africa.
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
Kama imepinduka hivi.. kumbe hapo nd’o iko sawa. Hujaipenda hii mtu wangu? Wenyewe wanaiita The Upside Down House, iko Poland.
Nitafurahi kuona umendikia nyumba ipi imekuvutia zaidi kati ya hizo

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni