.

Jumatano, 11 Mei 2016

Mtaalamu wa IT mwenye umri mdogo kuliko wote Duniani


Ayan Qureshi.
Ayan Qureshi.
Wazazi wengi Afrika wamekuwa hawajali kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi wanapokua kwenye hatua ya utoto na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni kwamba ukiongea na watu ambao wana vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo kama mpira wa miguu, ama kuimba na vinginevyo utagundua kwamba jitihada binafsi zimewaongoza kugundua vipaji vyao na mchango wa wazazi ni mdogo ama usiwepo kabisa.
Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake ambaye ni mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu.
Katika mahojiano na mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa na Microsoft ambaye ana umri mdogo zaidi duniani.
Hiki ndicho cheti alichopewa mtoto huyo na Kampuni ya Microsoft.
Hiki ndicho cheti alichopewa mtoto huyo na Kampuni ya Microsoft.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni