.

Jumatatu, 16 Mei 2016

KABAANG: WEMA SEPETU NA OMMY DIMPOZ KWA MARA NYINGINE TENA WAONEKANA KWENYE PICHA HIZI TATA

LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine ametengeneza habari, amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’,

Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika mapozi ya kimahaba huku Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake.

Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui.
“Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si mtu wa kutangazatangaza mambo yake na ndiyo maana hadi Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya hadi kumuimba kwenye wimbo wake,”kilisema chanzo

MAZINGIRA YA TUKIO

Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, picha hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani kwa Dimpoz, Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi wetu.

“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya maana wenyewe hawataki kuanika mambo yao,” kilisema chanzo hicho.

WEMA ASAKWA

Baada ya kupata ubuyu huo, Reporter wetu

‘alimvutia waya’ Wema ili kumsikia

anazungumziaje picha hizo na uhusiano huo

unaodaiwa ni wa siri, simu yake iliita bila

kupokelewa lakini baadaye rafiki yake mmoja

alisema huenda hakupokea kwa kuwa siku

hiyo alikuwa safarini kuelekea Dodoma.

“Jana (Jumatano) aliniaga ana safari ya

Dodoma so (hivyo) nafikiri yupo njiani na

wenzake na pengine kelele za wasanii ndani

ya gari si unajua tena na kaenda na wasanii

wenzake wengi tu,” alisema rafiki huyo

ambaye hakupenda jina lake lichorwe

gazetini.

DIMPOZ HUYU HAPA

Baada ya kumkosa Wema, Repoter wetu

alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha

hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake

lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.

“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga

hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si

nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia

lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua,

Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna

kitu kingine zaidi ya ushikaji. Kuna mtu

itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini

nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema

Dimpoz.

KUMBUKUMBU

Wema na Dimpoz walidaiwa kuanzisha

uhusiano wa kimapenzi, Februari, mwaka jana

walipokuwa wakirekodi video ya Ommy,

Wanjera nchini Afrika Kusini.

Picha zao ‘tata’ wakiwa chumbani zilizagaa

kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa

katika vyombo vya habari.

Baada ya hapo, Wema aliripotiwa kutembea

na wanaume tofauti akiwemo Idris Sultan,

mshindi wa Shindano la Big Brother Africa.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni