.

Jumatatu, 15 Mei 2017

Jokate Ahimiza ‘Mastaa’ Kurudishia Jamii

Mjasiriamali na Mwanamitindo maarufu nchini Tanzania, Jokate Mwegelo, amewaasa watu maarufu nchini Tanzania kujitolea kusaidia kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii ili kupunguza mzigo kwa serikali.

Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Wanafunzi wahitimu wa Jangwani Wikiendi iliyopita.
Jokate amesema hayo wikiendi iliyopita kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani .
Mrembo huyo ambaye ni Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa (UVCCM), amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo, lakini wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali husasani Elimu na Afya kwani hali ilivyosasa, ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote .
Jokate alisema Shule ya Jangwani ni Kongwe lakini mpaka sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi ambao kwa sasa wana nyadhifa na wanashindwa japo kujitoa kutatua matatizo ya Shule hiyo.
Mimi sijasoma Jangwani, lakini niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru viwanja kwa sasa vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine wasaidie, kuondoa changamoto zilizopo”,Alisema Jokate.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni