Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize Alhamisi hii amethibitisha kuachana na malkia wa filamu, Jacqueline Wolper.
Huwenda wawili hao wamezingua siku za karibuni, kwani Machi 16 mwaka huu Harmonize aliachia project yake ya wimbo ‘Niambie’ ambayo ndani yake Wolper alicheza vitendo na pia walishirikiana kwenye ishu ya promotion ya wimbo huo.
Akiongea katika kipindi cha Leo Tena, Harmonize amedai alikuwa na mipango mingi na Wolper lakini ameona bora aachane naye ili aupeshe shari.
“Sipo katika mahusiano, inshort kila mtu ana maisha yake ‘tumeachana'” alisema Harmonize .
Pia muimbaji huyo alikanusha taarifa za kwenye mitandao kuwa anatoka kimapenzi na msichana wa kizungu.
Hata hivyo hakuweka wazi sababu maalum ya kuachana na mpenzi wake huyo aliyedumu naye kwa muda mrefu pamoja na kumtambulisha kwao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni