Staa mwenye kiwango cha juu Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe amefunguka kuwa, wasanii wengi waliopo kwenye tasnia ya filamu ni wanafiki na wanafuata mkumbo, hawako kiuhalisia.
Akizungumza na Showbiz, wakati wa maandamano ya kupinga wizi wa kazi zao na uingizwaji na uuzwaji holela wa sinema za nje, Wolper alisema kuwa, wasanii wangekuwa na umoja wangeungana siku hiyo kwa ajili ya kujua hatima ya kazi zao wanazozifanya na zinazowaweka mjini, lakini kwa kuwa wengi ni wanafiki imeshindikana.
“Nachukizwa na unafiki Bongo Movi, kwa kweli unakera sana, hawako kiualisia ndiyo maana kufika tunapotaka ni ngumu sana,” alisema Wolper.
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv
Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni